Return To Message Board
Author Topic:   CCM MBAYA IIMETOA KIKWETE MBAYA
MUNISHI posted 7/9/05 6:20 AM    
Ndiyo. Nimeitwa kuikomboa Tanzania. Mungu keshawajibu Watanzania maombi yao. Ameniita Munishi niwakomboe ndugu zetu Watanzania kutoka minyororo ya CCM. Sasa nikisema hivyo wachache hawanielewi.Lakini maneno yako ya sasa naafikiana nayo. (Ila isiwe ni mahindi atupiwayo kuku anaswe) Kikwete ni wa CCM. Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Je ni haki kwa CCM kuumaliza upinzani jinsi hiyo Tanzania? Hatukatai pengine kuna mazuri ya CCM. Lakini kioo cha kuuona uzuri wa CCM kama upo, ni upinzani wenye nguvu. CCM Kutumia pesa za walipa kodi Tanzania kuumaliza upinzani hilo ndilo linaloniuma ROHO sana. Nasikia uchungu kiasi cha kuamuru ardhi ipasuke iwameze CCM.Huo ni ubinadamu ambao mimi ni sehemu yake. Uchungu wangu haumaanishi nawachukia CCM. Hapana. Lakini siyapendi wafanyayo.Kuninyima haki ya kujieleza Tanzania ni kosa ambalo CCM watalijutia milele. Kuzipiga marufuku kanda zangu ni sawa na kunifunga kinywa nisizungumze na Watanzania. CCM hawana haki ya kufanya hivyo. Kwamba wanatumia Polisi kuwasumbua wote wanaouza kanda zangu, wananifanya maarufu lakini kwa gharama ya kuwatesa watanzania wenzangu wasio na hatia. Hilo pia linanichoma kama kidonda moyoni.Kama nyimbo zangu zina lolote baya basi wa kuadhibiwa ni Munishi na siyo watu wasio na hatia. Kwani wanaogopa nini kuniweka kizuizini? Au ni lini wataitimiza ahadi yao ya kuniua? Niko tayari. Majuzi wamekuwa wakinifuata kila niendako. Wafanye waliokusudia kufanya kuliko kuwatesa Watanzania kwa kisingizio cha Munishi. Lakini ningekuwa mimi ni Serikali ya Mkapa, Ningetangaza kwamba Serikali ilikosea kupiga marufuku nyimbo za Injili alizoimba Mchungaji Munishi. Tena Serikali ingetoa Tamko rasmi la kumuomba Munishi msamaha na kukubali kumlipa hasara yote iliyosababishwa na Marufuku ya Serikali. Wakifanya hivyo siwezi kuwa mwana CCM, lakini pia watamaliza umaarufu wa Munishi. Lakini Munishi ni maarufu? Hapana. Ila Mkapa na CCM wamemfanya maarufu.Je Munishi anaukubali umaarufu huo? Hapana. Kisa ni kwa sababu CCM wanawatesa wengine wasiohusika na Munishi kumpatia Munishi umaarufu.Nimechanganya mengi, lakini la msingi ni kwamba Kikwete hatufai Tanzania.Sababu mnazijua wenyewe.Kikwete wa CCM hafai.CCM mbaya haiwezi kuwa na Kikwete mzuri.Tena Kikwete mzuri asingekubali kuwa CCM mbaya
Munishi posted 7/11/05 9:38 AM    
Wakati Waislamu wameanza kumshuku Kikwete, Wakristo nao wanasema kikwete siyo wao. Magazeti yenye misimamo mikali ya Kiislamu yamemtaka Jakaya Mrisho Kikwete atangaze msimamo. Ama aachane na Uislamu abatizwe awe Mkristo, au abaki Mwislamu. Walihoji kwamba kikwete hawezi kuwa na dini zote mbili. Yaani hawezi kuwa Mwislamu Mkristo. Nao Wakristo kwa upande ule mwingine wanashindwa kabisa kumwamini Kikwete kwani wanajua wazi kwamba yeye ni Mwislamu. Kwa Lugha inayoeleweka, Waislamu wanapomuona Kikwete na maaskofu, wanahisi kwamba huko amepewa nyama ya nguruwe awaletee msikitini. Nao Wakristo wanapomuona Kikwete kanisani kabla ya kubatizwa na kuukana Uislamu, Wanaona kama ametumwa na wenzao walete majini kanisani. Tayari Bwana Kikwete ana kibarua kigumu kuhusu imani yake kwa Mungu. Urais anautaka na Uislamu bado anaupenda. Ujanja wa wanasiasa kuwatapeli watu wa dini unafikia mwisho. Nyerere alifanikiwa kuwadanganya Watanzania kwamba CCM na serikali yake havina dini, Lakini baada ya Mkapa Mkristo kuwaua Waislamu Zanzibar, Watanzania wamejua kumbe serikali na CCM zina dini. Wanapotafuta mpaka wa dini na siasa wanakosa. Kwani wenye dini ndio wapiga kura. Tena kwa CCM kumteua Kikwete Mwislamu baada ya Mkapa Mkristo aliyekuja baada ya Mwinyi Mwislamu, Aliyechaguliwa na Nyerere Mkristo, sasa ni wazi kwamba dini mbili ndizo zinazopokezana uongozi Tanzania. Waumini wa dini nyingine wanaona wananyimwa haki na dini mbili ambazo zimeitawala Tanzania tangu tupate kile walichokiita UHURU. Kwa wale wasio na dini pamoja dini nyingine ambazo siyo Wakristo wala Waislamu, wakati sasa umefika nao wapewe nafasi ya kuiongoza Tanzania. Imegunduliwa kwamba Lugha ya Serikali haina dini ilitumiwa kuwapumbaza Watanzania kumbe kinachotawala ni DINI. Mbona baada ya Nyerere Mkristo alifuata Mwinyi Mwiislamu? Tena mbona baada ya Mwinyi Mwiislamu alifuatiwa na Mkapa Mkristo? Au tuseme yote ni bahati mbaya kwamba baada ya Mkapa, CCM wameona vyema wamteue Mwislamu Kikwete? Kama tutalazimishiwa Kikwete basi duara la Waislamu na Wakristo kuitawala Tanzania sijui litaishia wapi.Tunashangazwa na ukimya wa dini zilizoachwa nje ya uongozi huku wakidanganywa kwamba "Serikali haina DINI. Suluhu ni KATIBA iwaruhusu wagombea binafsi ili kila dini iteue mgombea wake. Magazeti ya kiislamu yana haki ya kujua kama kweli Kikwete wa CCM ni Mwislamu mwenzao. Badala ya magazeti ya Kikristo kuhoji kama Kikwete atalipiza kisasi cha Mkapa kuwaua Waislamu, wao wanapayuka hovyo. Mfano ni gazeti la "Habari Njema" Linalokosoa gazeti la kiislamu.
munishi posted 7/12/05 5:03 PM    
Kikwete wa Jakaya ni uteuzi wa CCM. Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Kwamba CCM wamemteua mtu wao, hiyo siyo sababu tosha kulifanya Gazeti la Kikristo kuanza kupayuka. Mbona? Habari Njema wanasahau kwamba wanasiasa ni WAONGO. Sasa wanalitapeli Kanisa. Badala ya Gazeti la kidini kuwaonya kondoo dhidi ya MBWA MWITU wanasiasa, Wao wanaanza kufurahia posho wanayotupiwa kama KUKU atupiwavyo mahindi kumbe yanaashiria mwisho wake. GTV Tumekataa kumeza ndoano ya CCM hata waweke chambo gani. Tutatumia kila lililo ndani ya uwezo wetu kuwaonya Watanzania wajihadhari na mnyama huyu CCM. Amewameza wenzetu kwa zaidi ya miaka arobaini, na sasa anatutapeli tumwachie nafasi aendelee kutumeza kwa miaka mitano ijayo. Haiwezekani, Hatukubali, Hatutaki, Tena tumekataa.Uhuru wa CCM kumteua Kikwete wa Jakaya, unapaswa kuishia pale uhuru wetu kuteuliwa kama wagombea binafsi unapoanzia. Kuanza kushangilia na kutumia pesa za walipa kodi kununua nafasi kwenye vyombo vya habari ili kutoa kauli za kiburi, Hakutaisaidia CCM. Ikiwa gazeti la kiislamu liliandika kwamba Waislamu hawamtaki Kikwete kwani ni kibaraka wa KANISA, "Habari Njema" Wangepaswa kumkemea Kikwete aache kulitumia Kanisa kwa manufaa yake kisiasa. Akifikiri anajitengenezea mazingara ya kukubaliwa na Wakristo, atajikuta pabaya. Waislamu wameanza tayari kumkana kwamba yeye kikwete si mwenzao. Wakristo nao sidhani kwamba watadanganyika na tabia ya ghafla ya Kikwete kuwa mgeni makanisani. Wengi wameanza kuifananisha tabia hiyo na pipi apewazo mtoto aache kulia. Wanasiasa Tanzania bado wanafikiri kwamba Watanzania ni watu wasioweza kuchambua mambo. Mwislamu Kikwete anapoanza kuingia kwenye majumba ya ibada {MAKANISA} bila kuukana uislamu ni sawa na kuwatania wenye imani hizo. Kifupi niseme "ANAKUFURU." Sambamba na hilo, Mkristo Benjamin Mkapa anapojifanya kuingia misikitini bila kusilimu awe Mwislamu, hiyo ni KUFURU kwa dini ya Kiislamu. Nasema hivyo kwa sababu wote wanajua nini kinapaswa kufanyika ndipo mtu awe muumini wa dini. Kuyakataa masharti ya dini husika na uingie humo ukiwa KAFIRI, kisha utoke humo ukiwa umewadanganya, hiyo inaonyesha kukosa adabu kwa Mungu anayeabudiwa na watu hao. Ikiwa wanasiasa hawawezi kuikosea adabu bendera ya nchi, Vipi wakose adabu kwenye sehemu za kuabudia??? Wanakuja makanisani na ahadi za uongo. Wachungaji na Mashehe wanakubali vipi wanasiasa waingize unajisi Makanisani na Misikitini? Sehemu Takatifu mnakubalije Kikwete aingie na uchafu wake na atoke akiwa amewachafua? Kulingana na imani ya Kikristo Kikwete Mwislamu lazima aukane uislamu ndipo apewe nafasi ya kufanya chochote Kanisani. Mambo ni hivyo hivyo Misikitini. Kafiri hawezi kuruhusiwa kuingia Msikitini akiwa amevalia viatu, huku amebeba nyama ya nguruwe. Hiyo ni KUFURU na kuikosea adabu KORAN TUKUFU. Wanasiasa wanapoingia Misikitini kwa lengo la kuwadanganya Waislamu wawaunge mkono, ni sawa na kuingia na nguruwe msikitini. Wanakuja na pesa za Rushwa na wanawanunua wakuu wa dini. Hilo ni kosa linalopaswa kukemewa na magazeti yote ya kidini. Tunalishangaa "Habari Njema" Gazeti la Kikristo kuanza kumpigia Debe Kikwete wa Jakaya na kusema ni wa wote. Wangefanya vizuri kusahihisha hilo na kusema Kikwete ni wa Jakaya na tena wa CCM. Watanzania wana mtu wao.Tunachoomba ni kwamba Watanzania wapewe nafasi ya kumchagua yule watakaeona anawafaa kuwaongoza. Kujaribu kuwalazimishia Kikwete, msishangae akiwa kiwete kama Mkapa. Nyerere alitulazimishia Mkapa, akatoka akiwa kiwete, Mkapa asijaribu kutulazimishia Kikwete kwani Mungu anajua nini cha kufanya na wale wanaowatesa Watanzania. Sina tatizo na uteuzi wa CCM, lakini namuomba Bwana Kikwete asije Kanisani kwangu kututapeli kwamba yeye anatupenda Wakristo. Ikiwa anaupenda kweli Ukristo, Kipimo chake ni aikubali Injili ya Yesu, Kisha amwamini Yesu badala ya Mtume Mohamad, Halafu tumbatize aitwe jina lolote hata kama akipenda kubaki na jina lake Kikwete hatuna tatizo hapo. Akikubali hayo tunamkaribisha kanisani. Lakini siyo aje kutuletea pesa za wizi.Huku akijifanya anachangia miradi ya dini ya Kikristo. Gospel TV tunaunga mkono gazeti lililomkosoa Kikwete na kusema kwamba Waislamu wamemshitukia Kikwete. Nasi GTV tunasema kwamba hata Wakristo wa kweli, Tumemshitukia Kikwete. Labda ajaribu mbinu nyingine. Lakini hii ya kuja Kanisani mwenye dhambi halafu aondoke ametuingiza dhambini tumeikataa sawa na tulivyomkataa shetani na mambo yake yote.
Return To Message Board

http://munishi.com  | Post New Topic