Return To Message Board
Author Topic:   KAKOBE ANATUIBIA WASHIRIKA FGBF CHURCH
Mshirika FGBF
(Moderator)
posted 2/27/04 2:28 PM    
Kakobe anatuibia washirika kwa michango inayolenga kumtajirisha mwenyewe. Washirika tunaendelea kuwa masikini wakati Kakobe anazidi kuwa tajiri kwa pesa za washirika.
Wenzangu mnasemaje?


http://munishi.com
http://munishi.com
Bruno Bernard posted 3/10/04 1:33 PM     Click here to send email to Bruno Bernard  
Mr.Munishi kama huna la kuongea nyamaza kimya!Siyo sifa kuongea hasa pale unapoongea kile usichokijua. Wewe ni mshirika wa FGBF tangu lini? Mimi kama mshirika wa FGBF ninapoona maneno kama haya ninajua ni maneno ya mpinga Kristo ambayo kwa wakati huu hayana nguvu tena!.Usipende kuzungumzia watu wengine;kwani washirika wa kanisa hilo hawaoni na wewe ndiyo unayeona?Acha kucheza na usichokijua,kama unahubiri Injili hubiri Injili,kama umeishiwa nyamaza kimya!Wengi wa jinsi yako sasa hivi wanajuta kwa kumnenea mtumishi wa Mungu mabaya.Sipendi kuelezea lolote kuhusiana na maada maana haina maana yoyote,unawaza pesa tu kama Yuda. Iskariote
Munishi posted 3/10/04 3:16 PM    
Bwana Bruno Munishi unamsakama wa nini? Anayelalamika hapa ni mshirika wa Kakobe.
Kama Kakobe kakutuma kumtetea, basi kanusha tuhuma na siyo kunisakama Munishi.
Ukumbi huu uko huru kwa mamilioni ulimwenguni kote kutoa madukuduku yao. Kama kuna wanaomtuhumu Kakobe, ni juu ya Kakobe kujibu tuhuma na siyo kukutuma kunisakama.
Niacheni nina mengi ya kufanya.
Bruno Bernard posted 3/12/04 9:52 AM     Click here to send email to Bruno Bernard  
Bwana Munishi,huyo unayedai kwamba ni mshirika angejitambulisha japo hata kwa jina, na akaelezea japo kwa muhtasari ni jinsi gani anachukuliwa hizo pesa zake na kuachwa masikini, na Kakobe mwenywe kuwa tajiri; vinginevyo inaonesha hayo ni majungu tu.Kanisa hili siyo shirika ambapo mtu anaweza kupokea mshahara na akadai kwamba ananyimwa mshahara wake, bali ni kanisa kama makanisa mengine.Watu wanatoa zaka na sadaka kwa ajili ya huduma mbalimbali za kanisa kama makanisa mengine.Huyo mtu kama imani ilimshinda asitafute visingizio.Kutokana na jinsi tulivyo washirika wa FGBF kama ninavyofahamu, hakuna mshirika aliye hai kiimani anayeweza kuzungumza habari za unafiki kama hizo. Kama ni mtu alikuletea habari kama hizo huyo kashindwa imani;hatunaye hapa, NAWE KAMA MTUMISHI WA MUNGU USIMSAIDIE WALA KUMSIKILIZA MTU WA JINSI HIYO ,MAANA ANAFANYA KAZI YA SHETANI!Watu ambao hawajaokoka wakiziona habari hizi wataokoka kweli? Si tutakuwa tumewazuia!Mungu akubariki,na pia Mungu atusaidie tusiingie katika mitego ya shetani bila kujua, maana adhabu haitatuacha kwa sababu ya kutokuijua sheria yake!,Amen.
Mshirika FGBF posted 3/13/04 3:30 PM    
Nasema KAKOBE ni mwizi. Michango kanisani haiishi, kinachofanywa na michango hiyo ni Kakobe kuamua kuzitumia pesa zetu apendavyo. Mara aamue kutumia mamilioni kununua zawadi kwa Kulola tapeli mwenzake, na pesa nyingine anazitumia kuishi kifahari kuliko wengi wetu ambao ndio tunaozitoa pesa zenyewe. Nisemayo hapa, Kakobe ni mkuu kuliko hata Yesu. Asemalo ndilo na hakuna wa kumuuliza. Kulingana na Biblia sote ni wanafunzi wa Yesu na Kakobe anatakiwa ajue hivyo. Mafundisho kwamba Mungu lazima aseme na Kakobe na wengine tufuate ni Uongo kutoka kuzimu. Kila mwamini mradi amezaliwa mara ya pili Mungu anazungumza naye kupitia roho mtakatifu. Kwenye kanisa letu FGBF Kakobe ndiye kila kitu. Tunataka iundwe kamati kanisani itakayopanga pesa za kanisa zitumike vipi. Washirika wahusishwe kuhusu matumizi ya pesa zao. Pia michango isiwe mingi kama ilivyo sasa. Wengi tumelazimika kuuza nyumba, viwanja, na magari ili tutoe sadaka kanisani. Iweje sisi tubaki bila magari wakati Kakobe anabadili magari kama soksi? Kipimo cha kukua kwa kanisa lazima kiwe washirika wangapi Mungu amekutana na mahitaji yao ya kila siku, na siyo utajiri wa mtu mmoja anayejiita askofu Kakobe. Wizi huu ndio tunaoukemea. Wengine wanasema kwamba watu wasiookoka wakisoma habari za kumkemea Kakobe hawataokoka. Hiyo siyo kweli. Badala yake wataokoka kwa wingi wakijua kwamba pesa zao zitakuwa salama kanisani na siyo kuishia kwenye mifuko ya matapeli kama Kakobe.
Ikiwa mitume walikemeana pale ukengeufu ulipoingia, Kakobe ni nani asiambiwe kwamba anapotoka na imani potovu ya kujifanya kwamba yeye ndiye pekee mtumishi wa Mungu na sisi wengine tusiulize chochote?
Wote tulioamini tumepewa uwezo wa kufanyika WANA WA MUNGU na ni wakati wetu kudai haki zetu wenyewe kwa Mungu. FGBL SITOKI. Nitadai haki zangu hapa. Kakobe ajue hivyo. Pesa zetu arudishe tufanye miradi ya kijamii kanisani. Madaraka aliyojivika ayavue. Katiba ya kanisa lazima ifuatwe na uchaguzi wa askofu ufanywe ili tumpate kiongozi mcha Mungu kanisani mwetu.
Bruno Bernard posted 3/15/04 8:04 AM     Click here to send email to Bruno Bernard  
Wewe unayejiita mshirika wa FGBF ni wa ajabu sana,tena sana!Hivi kwa mara ya mwisho umeenda kanisa la FGBF lini na kuna nini kinachoendelea huko hata sasa?Huogopi hata unachokisema?Roho wa Mungu anakushuhudiaje kuhusu maneno yako hata sasa?Hivi mtu mwizi mwenye kutafuta utajiri mahali panapodhaniwa kuwa ni kusanyiko la Mungu, anaweza akawa na Roho wa Mungu, hata Mungu akamtumia kwa miujiza na ishara kwa jina la Yesu? Au hata hiyo miujiza kwako ni ya shetani?Au hata wale wanaookoka ni wanafiki kama wewe?Mtu mwizi anaweza kuhubiri Injili kwa upako wa Roho Mtakatifu,na maneno take yakawa na nguvu za kuponya na kuokoa?Anasimama vipi kuhubiri wakati moyoni mwake anazo dhambi?Hivi wadhani kuhubiri neno la Mungu ni kama,siasa ambazo hazina hata maombi? Huoni kwa maelezo hayo hujui unachokitafuta hata kama unadai kuwa umeokoka na unasali katika kanisa hili? Maandiko yanasema tokeni kati yao mkatengwe nao, kuna urafiki gani kati ya nuru na giza!Hivyo kama umegundua kuwa Kakobe ni mwizi basi hapo ni giza kwako,maana mwizi mnafiki na tapeli atakukufundisha nini!;nakushauri tafuta kanisa unalodhani linalohubiri kweli ili uwe huru, vinginevyo huna unachokifanya zaidi sana unatenda dhambi za kumsikiliza unayedhani kuwa ni mwizi.Mimi siyo msemaji nimeingia katika mjadala huu,kwa sababu nimekerwa kuona mpaka leo hii wapo watu ambao wanadhaniwa kuwa wameokoka lakini bado hawajajua kupambanua nuru na giza.Sitataka kuendelea tena na hoja hii.Ndugu unayejiita mshirika wa kanisa la FGBF kwa heri, Bwana Yesu akufungue ili uache kumnenea mtumishi wa Mungu Kakobe mabaya,Ogopa!.Amen.
Mshirika FGBF
(Moderator)
posted 3/15/04 1:16 PM    
BRUNO UNAKOSEA KAKOBE NI TAPELI
Bruno unakosea. Kanisa ni mali ya Yesu na siyo mali ya Kakobe. Wakuondoka ni Kakobe siyo mimi. Wachungaji na maaskofu matapeli wamekuwa wakiufunika uoza wao kwa kuwatimua wanaojaribu kuwakosoa. Wanatumia lugha hiyo ya "kama kanisa la Kakobe limeoza ondoka uwaache na uoza wao." Ndiyo maana sitaki kutaja jina langu.
Kakobe atanitaja kanisani kama nimetengwa na kanisa ili kuzima tuhuma dhidi yake. Anajua wazi kwamba kanisa ni sawa na gari ya dala dala inayobeba na kushusha. Safari hii tumeamua kupigania haki zetu tukiwa kanisani FGBF. Hatutoki Kakobe ndiye atakayetoka. Katiba ya kanisa inaturuhusu kufanya hivyo.
Mimi nimeisoma Katiba na ndiyo maana washirika hatusomewi katiba ya kanisa inasemaje kuhusu askofu TAPELI. Kakobe ameifanya katiba ya kanisa kuwa siri kwani washirika tukiisoma tutazijua haki zetu kama waumini. Kanisa kama mwili wa Kristo ni mali ya Yesu. Kanisa la FGBF pamoja na mali zinazomilikiwa kwa jina la kanisa ni mali yetu waumini wote. Tuna haki ya kujua mapato ya kanisa ni kiasi gani, na yanatumika vipi.
Hiyo ni haki yetu kiroho na kisheria. Ndiyo maana tumeanza kuzidai haki zetu kiroho. Ikishindikana tutazidai kisheria. Hili siyo suala litakalomalizika kwa kuwatisha washirika. Kwamba watu wanaombewa na Kakobe wakapona isiwe kisingizio. Mwenyewe sina imani kwamba Kakobe akiniombea nitapona.
Mimi ndiye nikimuombea Kakobe atapona ugonjwa wa kupenda pesa na kujiona mkubwa kuliko hata Yesu mwenyewe. Huo ni ugonjwa. Lakini inapaswa ieleweke kwamba Mungu humponya mtu kulingana na imani ya mhusika kwa Mungu, na siyo kwa Kakobe. Ilivyo ni kwamba Mungu ndiye huponya na siyo Kakobe. Ikiwa mtu yeyote ataombewa na Kakobe, halafu aelekeze imani yake kwa Mungu, lazima atapona hata kama Kakobe ni tapeli.
Mungu huangalia imani ya mtu kwake na siyo vinginevyo. Mungu hawezi kuacha kumponya aliyemjia kwa imani eti kwa sababu Kakobe ni Tapeli. Hapana. Kakobe Mungu atashughulika naye kivyake, na kondoo wanaomfuata Kakobe bila kuzijua hila zake Mungu atawashughulikia kivyao. Kwamba wagonjwa wanapona FGBF haimaanishi Kakobe ni mkamilifu. Hii inamaanisha Mungu yupo na ahadi zake ni kweli. Haihusiani na utakatifu au utakavitu wa Kakobe. Bwana Bruno wacha kuwapotosha watu hapa. Kakobe ni TAPELI na lazima aondoke tufanye uchaguzi wa askofu mpya.
Mungu aliyemwita Kakobe kwenye utumishi, ndiye anayetaka washirika tuamke na tumpinge shetani anayetunyemelea akimtumia Kakobe. Neno la Mungu linasema tuzijaribu roho hata kama roho hizo ni za malaika. Sembuse Kakobe ni nani tusiijaribu roho iliyo ndani yake? Injili ya Kakobe haikubaliani na neno la Mungu.
Hilo linatosha kusema kwamba Kakobe alaaniwe kwani anapotosha injili. Injili siyo Kakobe awe tajiri na washirika tuwe masikini. Injili ni tuinuke wote. Uongo huu umeendelea sana Tanzania hasa kwenye makanisa ya kilokole. Washirika hawakai makanisani sana. Jambo ambalo linawapa mwanya wachungaji MATAPELI kuwadanganya. Wakiingia wanahubiriwa toeni mtabarikiwa, wanatoa na hawabarikiwi, yanawafika shingoni wanaondoka, au wanafukuzwa baada ya kuuliza kulikoni, Kakobe na matapeli wenzake wanaendelea kuwatapeli washirika wapya ambao hujiunga kutokana na matangazo ya kanisa husika kwenye vyombo vya habari. Tunataka wizi huu ukome.


http://munishi.com
Gazeti Injili Online
Mshirika FGBF
(Moderator)
posted 3/15/04 1:16 PM    
BRUNO UNAKOSEA KAKOBE NI TAPELI
Bruno unakosea. Kanisa ni mali ya Yesu na siyo mali ya Kakobe. Wakuondoka ni Kakobe siyo mimi. Wachungaji na maaskofu matapeli wamekuwa wakiufunika uoza wao kwa kuwatimua wanaojaribu kuwakosoa. Wanatumia lugha hiyo ya "kama kanisa la Kakobe limeoza ondoka uwaache na uoza wao." Ndiyo maana sitaki kutaja jina langu.
Kakobe atanitaja kanisani kama nimetengwa na kanisa ili kuzima tuhuma dhidi yake. Anajua wazi kwamba kanisa ni sawa na gari ya dala dala inayobeba na kushusha. Safari hii tumeamua kupigania haki zetu tukiwa kanisani FGBF. Hatutoki Kakobe ndiye atakayetoka. Katiba ya kanisa inaturuhusu kufanya hivyo.
Mimi nimeisoma Katiba na ndiyo maana washirika hatusomewi katiba ya kanisa inasemaje kuhusu askofu TAPELI. Kakobe ameifanya katiba ya kanisa kuwa siri kwani washirika tukiisoma tutazijua haki zetu kama waumini. Kanisa kama mwili wa Kristo ni mali ya Yesu. Kanisa la FGBF pamoja na mali zinazomilikiwa kwa jina la kanisa ni mali yetu waumini wote. Tuna haki ya kujua mapato ya kanisa ni kiasi gani, na yanatumika vipi.
Hiyo ni haki yetu kiroho na kisheria. Ndiyo maana tumeanza kuzidai haki zetu kiroho. Ikishindikana tutazidai kisheria. Hili siyo suala litakalomalizika kwa kuwatisha washirika. Kwamba watu wanaombewa na Kakobe wakapona isiwe kisingizio. Mwenyewe sina imani kwamba Kakobe akiniombea nitapona.
Mimi ndiye nikimuombea Kakobe atapona ugonjwa wa kupenda pesa na kujiona mkubwa kuliko hata Yesu mwenyewe. Huo ni ugonjwa. Lakini inapaswa ieleweke kwamba Mungu humponya mtu kulingana na imani ya mhusika kwa Mungu, na siyo kwa Kakobe. Ilivyo ni kwamba Mungu ndiye huponya na siyo Kakobe. Ikiwa mtu yeyote ataombewa na Kakobe, halafu aelekeze imani yake kwa Mungu, lazima atapona hata kama Kakobe ni tapeli.
Mungu huangalia imani ya mtu kwake na siyo vinginevyo. Mungu hawezi kuacha kumponya aliyemjia kwa imani eti kwa sababu Kakobe ni Tapeli. Hapana. Kakobe Mungu atashughulika naye kivyake, na kondoo wanaomfuata Kakobe bila kuzijua hila zake Mungu atawashughulikia kivyao. Kwamba wagonjwa wanapona FGBF haimaanishi Kakobe ni mkamilifu. Hii inamaanisha Mungu yupo na ahadi zake ni kweli. Haihusiani na utakatifu au utakavitu wa Kakobe. Bwana Bruno wacha kuwapotosha watu hapa. Kakobe ni TAPELI na lazima aondoke tufanye uchaguzi wa askofu mpya.
Mungu aliyemwita Kakobe kwenye utumishi, ndiye anayetaka washirika tuamke na tumpinge shetani anayetunyemelea akimtumia Kakobe. Neno la Mungu linasema tuzijaribu roho hata kama roho hizo ni za malaika. Sembuse Kakobe ni nani tusiijaribu roho iliyo ndani yake? Injili ya Kakobe haikubaliani na neno la Mungu.
Hilo linatosha kusema kwamba Kakobe alaaniwe kwani anapotosha injili. Injili siyo Kakobe awe tajiri na washirika tuwe masikini. Injili ni tuinuke wote. Uongo huu umeendelea sana Tanzania hasa kwenye makanisa ya kilokole. Washirika hawakai makanisani sana. Jambo ambalo linawapa mwanya wachungaji MATAPELI kuwadanganya. Wakiingia wanahubiriwa toeni mtabarikiwa, wanatoa na hawabarikiwi, yanawafika shingoni wanaondoka, au wanafukuzwa baada ya kuuliza kulikoni, Kakobe na matapeli wenzake wanaendelea kuwatapeli washirika wapya ambao hujiunga kutokana na matangazo ya kanisa husika kwenye vyombo vya habari. Tunataka wizi huu ukome.


http://munishi.com
Gazeti Injili Online
Mapunda S. posted 4/16/04 7:47 AM     Click here to send email to Mapunda S.  
Deal all..Ni wazo zuri kuwa na open board kama hii ambapo mtu anaweza ku-post maelezo yake yeyote jinsi aonavyo.Katika swala hili la kuwapeleka watu kwa Yesu yatupasa kuwa makini sana hapa.Mimi naona mtu huyu aliyeanzisha hii site anamakosa sana kwa kuwa huwezi kuiacha site hii bila ku-moderate. Kama hakuna moderator, site hii itafanana na Dar Hot Wire site ambapo asilimia 99 ya watu wanazungumzia masuala ya ngono, wakitumia majina yasio sahihi.Kama kweli site hii imetengenezwa kwa ajili ya kuwaleta watu kwa Yesu, basi lazima some kind of moderation ifanyike kwa email zote na subscribers. NI KOSA KUBWA SANA KUWAPOTEZEA MUDA WATUMISHI WA MUNGU KUTAFAKARI MANENO/MAMBO YASIO YA MSINGI.Kwa wewe uliyeanzisha hii forum, katika kila dhambi itokanayo na hii site, nawe unakuwa kwenye dhambi ya KUKUBALIANA NA HAO WAYATENDAO!..Kwa mfano, jamaa mmoja akaja kwako na akasema, "rafiki yangu, naomba unipe nafasi/muda kidogo tu katika chumba chako, ninae rafiki yangu wa kike nataka tuzungumze faragha" nawe ukampa chumba chako, nae akafanya uzinzi hapo, wewe nawe unakuwa kwenye dhambi ya KUKUBALIANA NAE.It is not fair just to allow people to subscribe with their fake names to your forum like this which is aiming on discussing very important message of GODJE ULIANZISHA FORUM HII ILI WATUMISHI WA MUNGU WATUKANWE? NA WEWE UNAONA NI SAWA TU, TENA UNAFURAHIA. HAKIKA YANGU MIMI, KATIKA SWALA HILI UMEKAA PABAYA.Nakushauli kuwa tengeneza site/forum hii ukifanya huhakiki wa kila mtu anayetaka kupost na pia ukichuja kila message kabla haijawa publishedKWAKO wewe unayemtukana mtumishi wa Mungu.Ninakushauli kwamba mtafute Mungu/Yesu maadamu anapatikana! Mtafute yeye peke yake, kwakuwa yeye ndie njia ya kweli na uzima. Kwa habari ya Roho Mtakatifu, unajua kuwa anasema na watu kila siku. Basi muulize huyo Roho kwa habari ya mambo haya ili upate uhakika kwa maisha yako. Katika siku ile ya mwisho, wala hutakuwa nami, wala Munishi, wala Askofu Kakobe, ila ni wewe peke yako. Hakuna mshauri anaefaa hapa duniani kupita Roho Mtakatifu. Nae ndie atakayekushuhudia kwa habari ya haki dhambi na hukumu! Usitafute uwashilikisha wengine katika jambo usilokuwa na hakika nalo. Kwakuwa kama linakukera, hilo la kutoa basi liache. Mpaka hapo yule Roho atakapokushuhudia kwa habari ya utowaji, basi utatoa.Usitetee mali ukaona inafaida. Wala hakuna jema chini ya jua. Ulivyokuja ndivyo utakavyoondoka. Ulikuja bila nguo, utaondoka bila nguo! Ulikuja ukabebwa, utaondoka umebebwa.MUOGOPE MUNGU NA MAMBO YAKE, kwa kuwa upanga upo mkononi mwako. Chunguza maandiko katika kila jambo.


http://www.netsoltz.com
John sagamiko posted 5/11/04 6:01 PM     Click here to send email to John sagamiko  
samahanini mimi ni muumini wa asemblis of god lakini sijakubaliana na jambo la huyo mtu anaejiita muumini wa kakobe kwani huyo mimi na hisi ni kati ya wale walio na lana ya fedha kwani muda mwingi uliopita mimi nimesikia kuwa kakobe mwizi ana waibia waumini wake angalieni sana moto utawachoma ninyi kwa uchungu kwani nanyi mnaboliti kubwa machoni sasa hao wazee wa kanisa wanao kula sadaka humo makaniasani mwenu ndio sio wezi kumbuka ya kwamba yuda alimsaliti yesu kisa fedha hizo ndizo zinazo kuchoma wewe sasa kama unaamini kuwa kakobe anakula lushwa hata wewe munishi ni mla lushwa mkubwa mama lwakatale ni mlalushwa mkubwa na hata mwakasege mla lushwa mkubwa kupita kakobe na hata utakasilika huo ni ikweli usio fichika na chuki mlizo nazo zitawaua na kuwapeleka motoni angalia sana wewe na hao watu wako kwa maono nilioyaona mimi huyo anae jiita mshilika wa kakobe sasa mwenyewe wala hawa jali kabisa sasa ninyi ni machizi tafadhali eneza injiri sio chuki zilizo jaa kinyongo kama ni maswala yenyewe ndio hayo basi hata hizo dini msieneze tena bola mkajichanganye na makahaba na wachawi katika dunia iliyojaa uchafu wewe munisi kama unaweza ukimaliza kusoma balua hii upige magoti na kutubu sasa hivi mheshimiwa naomba mtubu mapema bluno usijali ukibishana na wadunia watakukosesha yambingu? hata mwalabu anakwambia kuwa ("Sammin kalbak yaakulak")yani ukimnenepesha mbwa wako basi atakuja kukula mwenyewe kwahiyo huyo mtu anae jiita muumini wa kakobe basi ni mbwa alinenepeshwa kwani wengi tunao makanisani mwetu wanatoka kwa kakobe na wakija makanisani mwetu wanapewa uchungaji kwa nini wakati kakobe ni mwizi na ni mwongo sasa chunga sana wewe na nhuyo mwenzi sasa moto umesha washwa na unakolea bado sisi tu kuchomwa tu na uongo tunao usema humo mitaani wewe kama kakobe anakula hela za kanisa anzipeleka wapi na nyumba anayoishi iko hivyo toka miaka ya tisini mpaka leo yeye anagali moja tu nissani wakati ninyi mnatembelea maplado na mesidis za wazungu na sadaka tena mantembea na waimba kwaya wenu mpo hapo ninyi sasa mimi nahitaji ujilekebishe wewe si muumini wa kakobe wala wadini ya kiklisto wewe ni mchawi unaye sukwa sukwa na mapepo yanayo kusumbua chunga sana mdomo wako wewe


http://www.biznas.com/sm
www.darhotwire.com
Adeline Siame posted 5/19/04 8:05 AM     Click here to send email to Adeline Siame  
Samahani, waachani wachungaji wa kondoo wa bwana msiwasakame, sio Kakobe atakayekufikisha mbinguni bali ni imani yako ndo itakufikisha mbinguni. Hakuna sababu ya kuhukumu, kwani mambo tunayoyafanya hapo duniani tutayakuta mbinguni, kwa kuwa kila mtu matendo yake yatamfuata. Kakobe endelea na imani uliyopewa na Mungu wako, wavute kondoo wa Bwana shambani mwake hasa kipindi hiki ambacho kinaonyesha wazi kwamba ndo nyakazi za mwisho.
Theophil Ruambo posted 5/26/04 7:25 AM     Click here to send email to Theophil Ruambo  
Ndugu unayesema Kakobe anatuibia kanisani, naomba nikuulize swali, umetoa nini hata Kakobe amekuibia? na tena utampaje mtu kitu wakati unamjua yeye ni mwizi? . Naomba ufanye uchunguzi kwa kuangalia maendeleo ya kanisa! makanisa ambayo wachungaji ni wezi yanadumaa kwani pesa zinaingia mifukoni mwao badala ya kutenda kazi ya Mungu. Wewe binafsi unayapimaje maendeleo yaliyopo katika kanisa la FGBF?. Pia kwa habari ya kumpa zawadi mtumishi wa Mungu Moses Kulola, hilo halina mjaladala kwa mtu aliyeokoka, wengi katika Biblia wamewapa vitu vya thamani watumishi wa Mungu kwa mfano mdogo nitamtaja mfalme Daudi na mwanae Sulemani.Bwana Yesu amesema ukitaka kupata thawabu ya Nabii basi mpe angalau maji ya baridi.Kwa hiyo kuwapa vitu, fedha, gari, makochi, nyumba watumishi ni jambo linaloubariki sana moyo wa Yesu japo kwa wanadamu wachache na shetani litawauma sana!
Mshirika FGBF posted 7/8/04 3:43 PM    
Mimi ni mshirika FGBF. Tangu nijiunge kanisani hapo, nimekuwa nikitoa matoleo. Majuzi niliuza gari na kiwanja kuchangia kongamano la wachungaji. Nasema Kakobe ni mwizi kwani pesa zote huamua mwenyewe azitumie vipi. Mbaya zaidi nimegundua kwamba Kongamano lile halikuwa likihusu kanisa na kukua kwake kama tulivyodanganywa.La Muhimu ni kwamba mimi sitoki FGBF. Kakobe ndiye anaetakiwa atoke kanisani kwani wizi wake sasa umezidi na hauvumiliki tena.
Maggy posted 7/14/04 9:53 AM     Click here to send email to Maggy  
mnaona!!! mnaanza kugombania pesa, huu umasikini unaowafanya kukimbilia kwenye ulokole mungu atawachoma mara mia, nani kakwambia fungu la kumi mpaka uuze gari/shamba ndo upeleke huko ulikopeleka? fungu la kumi linatoka tu pale kwenye kazi za kila siku sio uuze uwe masikini. Pole kaka kama umeuza gari lako hakuna cha kuokoka wala nini mwamini mungu na tumia busara sana sio watu kushika bible na wewe kufuata mkumbo
Bruno Bernard posted 8/6/04 1:43 PM     Click here to send email to Bruno Bernard  
Nimegundua kuwa, kumbe wewe unayejiita mshirika wa FGBF ni mpelelezi tu,unataka kujua iwapo ni kweli washirika wa FGBF wanajitoa kiasi hiki kama inavyosikika au la! Umetafuta njia hiyo ili uone ni nani atakuunga mkono ili upate habari kamili.Ndugu yangu ukweli ni kwamba Mungu hapelelezwi,jipeleleze kwanza wewe ndipo upeleleze na wengine.Ninavyofahamu mimi na ninavyoona ni kwamba FGBF hakuna anayeibiwa ila Watakatifu wa Mungu wapo kazini; wanautafuta ufalme wa Mungu kwa kuwaleta watu kwa Yesu.Kile wanachojitoa kinafanya kazi ya Mungu;ujenzi wa nyumba ya Mungu,kueneza injili kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwa njia ya televisheni nk.,ndiyo maana unaona kanisa linakua ;washirika wana hofu ya Mungu kuanzia Kakobe mwenyewe hadi chini, kila mtu anajua anachokifanya. Hata hivyo unatakiwa kujua kuwa, maeneo kama haya shetani hakosi,anawatumia mafarisayo ili kumwangamiza Yesu, lakini hawezi. Ole wako kama ni miongoni mwa mafarisayo, maana mpaka sasa hawajamtambua masihi kuwa ndiye aliyekuja kwa ajili yao!.Huyu ndiye masihi anayeshuka kwa ajili yako, safisha macho yako upate kuona, mpe Bwana Yesu maisha yako, Yeye ajaye anakua wala hatakawia,huu siyo wakati wa dhihaka. Nakuhurumia kwa maana umesimama kama kiambaza kuzuia hata wanaotaka kuingia, nao wamedanganyika kwa ajili yako, nao wamesema kama wewe kuwa hakuna kuokoka duniani, ndiyo maana hutaki kutaja hata jina lako.? Hivi ni nani anayeweza kutoa sadaka kwa Mungu na hatimeye aanze kujilaumu? Mtu huyo amepata kweli kuonja vipawa vya Mungu?Anakuwa anajua anachokifanya kweli? Nawe ndugu yangu acha kumpeleleza, Mungu okoka sasa, maandiko yanasema katika (Mathayo 1:21..... maana yeye ndiye atakayewaokoa watu na dhambi zao)Siku za mwisho utayatolea hesabu haya yote.Nilisema kuwa nisingeandika tena, baada ya ile foram iliyopita lakini baada ya kugundua kuwa wewe ni mpelelezi tu nimeona nikueleze kuwa upelelezi wako umegundulika, sisi tunajuana bwana! hakua lugha hiyo FGBF, hiyo ya kwako ni lugha ya kigeni! Mtu anayefikia hatua ya kujitoa kiasi hicho cha kuuza hata nyumba na mashamba kama ulivyodai halafu awe hana ufahamu wa neno la Mungu kiasi hicho,na aanze kuropoka ropoka namna yako, hakuna!!Hata hivyo unatakiwa kujua kuwa neno la Mungu linatukataza utani, kama wewe unafanya dhihaka kwa hayo unayoandika basi ole wako,(zaburi 1:1) mimi sipo katika utani, ninasema yale yaliyo moyoni mwangu.
Mshirika FGBF posted 8/8/04 8:19 AM    
Jamani si mnasikia? Kwamba wote wanaotoa mali zao kwa Kakobe hawawezi kurudiwa tena na fahamu zao waanze kudai mali walizoibiwa kwa kisingizio cha kumjengea Mungu nyumba. Hii inaonyesha wazi jinsi Kakobe anavyojiamini katika utapeli wake. Yaani washirika wameharibiwa bongo zao kiasi kwamba hawafikiri tena. Tunapojaribu kuonyesha jinsi Kakobe alivyo mwizi, tunaitwa majina mengi. Nasema ni afadhali mwizi anaetumia bunduki, kuliko Kakobe anaetumia neno la Mungu kutuibia. Mwizi wa Bunduki atakuibia siku moja na akuache, lakini Kakobe anatuibia kila siku na mbaya zaidi anaiba mpaka bongo zetu. Imefikia mahali kwamba hata wake zetu hawatusikii tena. Wanamsikiliza huyo anaejiita masihi wa Mungu. Nisemayo hapa ni kwamba haitasaidia kuniita mpelelezi, lakini Kakobe hatumtaki kanisani tena. Kama ni kweli wanaotoa watabarikiwa mara dufu kama Kakobe anavyotudanganya, basi mimi ningekuwa tajiri sasa. Badala yake nimekuwa masikini kuliko awali, na mchungaji sasa wala hanijali wala hana mawasiliano nami. Nilipokuwa nazo kila siku lazima anione anisalimu na ikiwezekana tuombe pamoja. Lakini sasa hata nikitaka kumuona inakuwa vigumu sana. Walinzi wake wanasema mchungaji yuko bize sana.Kama mafundisho ya Kakobe ni kuwafilisi wale walio navyo na kuwatafuta wengine walio navyo, kanisa litaendelea vipi? Sipingi kutoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, na pengine ndio maana ilikuwa rahisi kuingia kwenye mtego wa Kakobe. Lakini kile nimegundua ni kwamba makanisa mengi na la Kakobe likiwa mojawapo, ni mali za watu na siyo taasisi ya kuwaelekeza watu kwa Mungu kama ilivyopaswa kuwa.Makosa tunayofanya washirika ni kwamba tukigundua makosa hatusemi. Au hata baada ya kusema tukikemewa kidogo, tunaondoka na kumuacha mwizi aendelee kuwaibia wengine.Safari hii nimeamua lazima niwaelimishe wengine ili tumtoe mwizi na siyo sisi tukimbie kutoka kanisani. Nimeanza kampeni za kuwaelimisha washirika wenzangu kuhusu haki zao. Mungu ndiye aliyetuokoa na kanisa ambalo ni mwili wake linapaswa kuwa mali yake na siyo mali ya Kakobe.Sisi wote tuliomwamini Yesu na kutubu dhambi zetu ni wanafunzi wa Yesu, na Kakobe akiwemo. Kwa hiyo ni makosa kuanza kumwabudu Kakobe kwani yeye hajatuzidi chochote.Lazima mali za kanisa zijulikane zinatumiwa vipi na jumuia husika, na siyo Kakobe awe mwamuzi wa mwisho wa matumizi ya pesa zetu. Tunataka washirika wajulishwe wametoa kiasi gani na zilitumika vipi. Tena hakuna sababu ya Kakobe kukalia kiti ccccha uaskofu kwa miaka yote. Lazzima tufanye uchaguzi ili tumcchague askofu mpya.Kwa hiyo mawazo ya kwamba nitatoka kanisani ili Kakobe aendelee kuwaibia wengine kama mimi, mfute. Kakobe ndiye atakaetoka.Wakati wa kumtumia Mungu kunitisha umekwisha. Mungu ni baba yetu sote, na Mungu hapendi jina lake litumiwe na watu kama Kakobe kutuibia mali zetu, bongo zetu, na nani ajuae kesho tutaibiwa nini kama si wake zetu na mabinti zetu???? Lazima tabia hii ikome. Na itaanzia FGBF.
amani posted 11/24/04 10:01 AM    
Nilipokuwa mdogo nilijifunza neno moja katika biblia; ...na alaaniwe amneneaye mabaya mtumishi wa Mungu...Neno hili limenifanya niwe mwangalifu sana katika kila ninalosema juu ya mtumishi wa Mungu. Huenda wengine hawajalijua hili na ndiyo maana wanathubutu kuwaita watumishi wa Mungu eti matapeli bila kuwa na ushahidi. Nimemfahamu Askofu Kakobe tangu 1997 nilipotembelea fgbf Mwenge. Tangu, na hata kabla ya hapo, kulikuwa na uzushi dhidi yake hususani kutoka kwa waumini wa makanisa ya 'kiroho'. Wengi wao hawakuujua ukweli na wakaendelea kudanganywa kupotoshwa hata na baadhi ya wachungaji wao waliomchukia Kakobe. Binafsi niliijua kweli toka 1997 kwamba Kakobe ni mtu mwema, mwenye mzigo na kazi ya Mungu na ni mtu ambaye Mungu ninaye muamini kwa japo ndogo imani, amemkubali na kumpa kibali kuwa mjumbe wake. Nilifurahika sana pale wachungaji na maaskofu wa Kipentekoste walipo kaa pamoja na kurudisha umoja kati yao katika kongamano la maaskofu. Hii ilileta ufahamu na mtazamo mpya juu ya Kakobe hususani kwa wale ambao hawakuujua ukweli. Hapo mwili wa Kristo ulijengwa. Tafadhali ndugu zangu tusirudi nyuma, tukaleta tena habari za uzushi na utani dhidi ya mtumishi wa Mungu, ambaye usiku na mchana anaomba kwa kuugua ili tu mimi na wewe tupate afya, ili nchi yetu iwe na amani, haya yote yako dhahili. Kama ukumbi huu ni wa neno la Mungu, basi utumike kwa jinsi hiyo. Yesu anawapenda wahuni, hata Kakobe anawapenda wahuni, lakini hii haimaanishi kuupenda uhuni. Yesu anataka wahuni wabadirike na ndiyo maana anawapenda, na Kakobe anawapenda na kuwaalika hao ili awalete kwa yesu. Sasa unapokwenda kwa yesu ni vema uuache uhuni, kwani huwezi kuuleta uhuni nyumbani mwa Mungu. Kutukana watumishi wa Mungu ni uhuni mkubwa ambao unapaswa kuachwa mara moja.
TOBA posted 11/24/04 12:28 AM    
Acheni kutisha watu na LAANA. Kama mtu anasema ukweli atalaaniwa vipi? Mnanikumbusha wimbo wa wachungaji wengi siku hizi. Wanazini na wake za watu, na wanasema wasinenewe mabaya. Eti ni watumishi wa mungu. Watu kama kina Kakobe siwezi kuwaita watumishi wa Mungu. Kama kuna kasoro wanachotakiwa kufanya ni kutubu na siyo kuwatishia watu na LAANA hapa. Kama kulaaniwa watalaaniwa wao.
Rafa posted 11/29/04 6:26 PM    
Usielewe vibaya kuhusu laana. Ni kweli imethibitika mara nyingi tu kwa wachungaji na watumishi wengine kuwa wamefanya uzinzi. Hao amabo ushidi upo wanastahili lawama. Sasa mwenzangu, una ushaidi gani kama Askofu Kakobe kafanya hayo yanayosemwa, au unaamini tu kila unalosikia.Kama kweli unataka kuwa sahihi fanya uchunguzi binafsi ujue ukweli, vinginevyo unajiongozea mzigo wa dhambi.
Brian kithuku posted 11/29/04 9:49 PM     Click here to send email to Brian kithuku  
Mimi nawashauri wote mnaobishana kuhusu Kakobe mwende mkatubu dhambi zenu, mumfuate Mungu aliye hai kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia. Mmejichanganya bure na mambo ya madhehebu, sasa mnaona matokeo yake. Huo ulokole feki mnaoigiza ndio utakaowapeleka jehanamu, halafu mtashangaa sana mtakapokuta kwamba wale mnaodhani ni wadhambi wako mbinguni wanamshangilia Bwana! Tubuni na kuiamini injili. Hakuna njia nyingine ndugu zangu. Ikimbieni dhambi nayo itawakimbia. Tumsifu Yesu Kristu.
PETER posted 3/22/06 3:27 PM     Click here to send email to PETER  
Wote wenye wasiwasi na kakobe na huku wanajiita wakristo, ndio wale ambao biblia inasema nyakati za mwisho wengi watajitenga na imani wakifuata roho zidanganyazo, wakitafutia walimu makundi makundi lakini huku wakichomwa roho zao na kile wanachozungumzia. watu hawa ambao hukumu ya Mungu haitakawia juu yao maana masikio yao ni ya utafiti. wapo kwaajili ya kutimiza unabii wasikupe shida sana.
Santy Kimaro posted 9/5/06 9:42 AM     Click here to send email to Santy Kimaro  
Munishi Mungu wa Israeli bado anakupenda. Acha kabisa kuwanenea watumishi wake vibaya. Angalia ni wapi ulikoanguka utubu madamu muda ungalipo. Tafakari sababu za kuanzisha website hii.
Janet posted 9/5/06 4:38 PM    
Kimaro una akili timamu kweli? Kakobe ameanzisha kanisa la utapeli Dar. Waliotapeliwa wameanza kulalamika wasaidiwe na serikali ikiwezekana. Sasa wewe unakurupuka na kusema Munishi atubu. Dhambi gani Munishi aliyoitenda? Kuanzisha Website? Mbona hilo ni jambo zuri linalopaswa kupongezwa? Watanzania mko dunia gani? Yaani Kakobe akikosolewa ni dhambi? Namshauri Munishi aendelee na moyo huo wa kulisafisha kanisa la Mungu ili matapeli kama Kakobe wasipate nafasi ya kuwaibia watu wakitumia neno la Mungu.
Prince CHARLES posted 10/17/06 3:30 PM    
Ama kweli siku za mwisho zimefika... Nadhani Bwana Munishi na jopo lako amefanikiwa kufanya research ni namna gani KAKOBE anavyopingwa na kusapotiwa, ahsante kwa hilo nadhani umeridhika na utafiti wako huo na umeshajua ya kwamba hauko peke yako, unayempinga mtumishi wa Mungu huyo, sasa ni zamu ya kutoa maada ya kumjadili mchungaji wako kama na yeye ni mwizi, jambazi, au tapeli. Hivi unajua kwamba MUNGU anamuheshimu KAKOBE wewe u nani unayemdharau na kumbeza mpakwa mafuta wa Bwana, Yaani hii neema kidogo aliyekupa MUNGU ya kuwa na uwezo wa kufungua website ndio una FANYA MAMBO HAYA? ushauri wangu kwako kabla hujaharibu zaidi ruhusu na anzisha maada zitakazo wafanya watu waache uovu na kutenda mema, pia kama ni kweli upelelezi wako umeona ya kwamba KAKOBE ni mwizi na una ushahidi wa kutosha nenda kamshitaki ili afungwe, na kama unafanya hivi kwa challenge tu ACHA MARA MOJA NA UTUBU. Elewa punde Bwana atakuuliza nini umefanya ulipokuwa hapa duniani. Si kwamba nakuchukia bwana MUNISHI la hasha NAKUPENDA.
Mmachinga posted 10/20/06 2:30 PM    
Acheni kuwatisha watu kwamba Kakobe amepakwa mafuta.Mungu ni Baba yetu sote.Machoni pake sote ni sawa.Tulikuwa wenye dhambi tukasamehewa kwa neema.Suala la kumfanya Kakobe nusu Mungu,asiyekosolewa ni kosa.Ushahidi kwamba Kakobe ni Tapeli uko wazi.Tunangoja Polisi Tanzania wachukue Hatua za Kisheria. Wanaolalamika kutapeliwa na Kakobe ni wengi.Akikamatwa kwa tuhuma za kuwaibia Watanzania mali zao akitumia neno la Mungu, ndipo mtakapowaona waliot5apeliwa kwa macho. Tunamuomba Munishi na GTV yake waje Tanzania kuchukua picha za Tapeli Kakobe akiwa Gerezani Ukonga.
Mshirika FGBF posted 10/28/06 4:25 PM    
Nawashukuru wote mlionielewa. Nia yangu ni kuukomesha utapeli makanisani. Tunataka wakristo wazijue haki zao.Kwamba wote wanaotoa mali zao kwa Kakobe hawawezi kurudiwa tena na fahamu zao waanze kudai mali walizoibiwa kwa kisingizio cha kumjengea Mungu nyumba. Hii inaonyesha wazi jinsi Kakobe anavyojiamini katika utapeli wake. Yaani washirika wameharibiwa bongo zao kiasi kwamba hawafikiri tena. Tunapojaribu kuonyesha jinsi Kakobe alivyo mwizi, tunaitwa majina mengi. Nasema ni afadhali mwizi anaetumia bunduki, kuliko Kakobe anaetumia neno la Mungu kutuibia. Mwizi wa Bunduki atakuibia siku moja na akuache, lakini Kakobe anatuibia kila siku na mbaya zaidi anaiba mpaka bongo zetu. Imefikia mahali kwamba hata wake zetu hawatusikii tena. Wanamsikiliza huyo anaejiita masihi wa Mungu. Nisemayo hapa ni kwamba haitasaidia kuniita mpelelezi, lakini Kakobe hatumtaki kanisani tena. Kama ni kweli wanaotoa watabarikiwa mara dufu kama Kakobe anavyotudanganya, basi mimi ningekuwa tajiri sasa. Badala yake nimekuwa masikini kuliko awali, na mchungaji sasa wala hanijali wala hana mawasiliano nami. Nilipokuwa nazo kila siku lazima anione anisalimu na ikiwezekana tuombe pamoja. Lakini sasa hata nikitaka kumuona inakuwa vigumu sana. Walinzi wake wanasema mchungaji yuko bize sana.Kama mafundisho ya Kakobe ni kuwafilisi wale walio navyo na kuwatafuta wengine walio navyo, kanisa litaendelea vipi? Sipingi kutoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, na pengine ndio maana ilikuwa rahisi kuingia kwenye mtego wa Kakobe. Lakini kile nimegundua ni kwamba makanisa mengi na la Kakobe likiwa mojawapo, ni mali za watu na siyo taasisi ya kuwaelekeza watu kwa Mungu kama ilivyopaswa kuwa.Makosa tunayofanya washirika ni kwamba tukigundua makosa hatusemi. Au hata baada ya kusema tukikemewa kidogo, tunaondoka na kumuacha mwizi aendelee kuwaibia wengine.Safari hii nimeamua lazima niwaelimishe wengine ili tumtoe mwizi na siyo sisi tukimbie kutoka kanisani. Nimeanza kampeni za kuwaelimisha washirika wenzangu kuhusu haki zao. Mungu ndiye aliyetuokoa na kanisa ambalo ni mwili wake linapaswa kuwa mali yake na siyo mali ya Kakobe.Sisi wote tuliomwamini Yesu na kutubu dhambi zetu ni wanafunzi wa Yesu, na Kakobe akiwemo. Kwa hiyo ni makosa kuanza kumwabudu Kakobe kwani yeye hajatuzidi chochote.Lazima mali za kanisa zijulikane zinatumiwa vipi na jumuia husika, na siyo Kakobe awe mwamuzi wa mwisho wa matumizi ya pesa zetu. Tunataka washirika wajulishwe wametoa kiasi gani na zilitumika vipi. Tena hakuna sababu ya Kakobe kukalia kiti ccccha uaskofu kwa miaka yote. Lazzima tufanye uchaguzi ili tumcchague askofu mpya.Kwa hiyo mawazo ya kwamba nitatoka kanisani ili Kakobe aendelee kuwaibia wengine kama mimi, mfute. Kakobe ndiye atakaetoka.Wakati wa kumtumia Mungu kunitisha umekwisha. Mungu ni baba yetu sote, na Mungu hapendi jina lake litumiwe na watu kama Kakobe kutuibia mali zetu, bongo zetu, na nani ajuae kesho tutaibiwa nini kama si wake zetu na mabinti zetu???? Lazima tabia hii ikome. Na itaanzia FGBF.
MUNISHI posted 11/8/06 1:35 PM    
Kuna watu wanaosema nifute yale mabaya yote yanayosemwa kuwahusu watumishi wa Mungu, nia yale mazuri tu. Pengine kwa maoni yao wako sawa. Lakini mimi kama Mhariri siwezi kufanya hivyo. Kwani Kufanya hivyo ni kuwanyima uhuru wa kujieleza. Hatuna hakika kama tuhuma zao ni za kweli au uongo. Lakini kwa sababu nafasi ya kujitetea ipo, wanaoona wameonewa waje wajitetee nasi pia tutachapisha maoni yao bila kutoa hata neno moja. Website ya Injili haipaswi kuandika mambo ya upande mmoja. Ikiwa Biblia yenyewe inaandika habari za shetani akimjaribu Yesu, mbona unataka website ya Injili iandike yale mazuri ya Kulola na Kakobe na siyo yale mengine kama yapo? Hatuungi mkono kuharibiana majina bila sababu za msingi, lakini pia hatuwafungi mdomo wenye madukuduku yao wasiyatoe. Kazi ya website hii ni kuhakikisha kanisa la Mungu ni safi. Kama wewe siyo Kulola au Kakobe, kuwatetea unafanya kazi bure. Pengine yale unayofikiri hawakufanya, wanahukumiwa nayo kwani huenda walihusika katika yale wanayotuhumiwa kwayo. Ni mpaka waseme ndipo watu wanapoweza kunyamaza.Wao wanafikiri wasipojibu yataisha. Website siyo kama gazeti la UHURU. Habari ikiandikwa kwenye gazeti la UHURU inaisha siku hiyo hiyo na jioni gazeti hilo litafungia nyama, au kuwekwa msalani watu wachambie. Sivyo habari iliyoandikwa kwenye mtandao. Kadiri unavyoidharau, ndivyo inavyozidi kuwafikia watu wengi. Ushauri wangu kwa Kulola, ni kwamba aandike habari za kukanusha tuhuma hizo haraka. asipofanya hivyo atajilaumu mwenyewe kwani watu wataamini kwamba kweli yeye ni kama yasemwayo hapa. Lisemwalo lipo kama halipo laja. Huo ni msemo tu.
Edna posted 3/7/07 9:08 AM    
HABARIASKOFU KAKOBE NA DOLE KWA WACHONGA DOMO Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship -FGBF, Zakaria Kakobe ametahadharisha Wabongo wanaomchafulia jina wajiandae kuburuzwa mahakamani kudaiwa mamilioni ya fedha zitakazotumika kuendeleza kanisa lake. Kakobe alitonya kuwa amechoshwa na tabia ya baadhi ya wanaodai yeye ni bonge la tajiri anayewakomba waumini wake vitu kama fedha mikufu ya dhahabu hereni na pete zao wanapotinga kanisani kwake. Katika kufuta kabisa uvumi huo Askofu Kakobe alionyesha waziwazi kwenye kituo cha TV cha Channel Ten nyumba yake anayoishi iliyoko Kijitonyama jijini Dar. Akifafanua kila kilichokuwa kinachoonekana katika nyumba hiyo ya kawaida kabisa, alitonya kuwa hata vitanda vya watoto aina ya double decker amenunua karibuni kwani watoto wake walikuwa wanalala sebuleni kwa kukosa pa kulala. Aidha alionyesha vilevile chumba chake cha kulala kilichokuwa kimejaa masanduku yaliyopangwa nguo kutokana na udogo wa kabati lililokuwa ndani ya chumba hicho. Alitonya vilevile kuwa gari pekee anayomiliki ni pick up iliyokufa iliyokuwa mbele ya nyumba yake na kwamba gari anayotumia aina ya Nissan Patrol ni mali ya kanisa la FGBF. Alimalizia kuwa mwenye ushahidi wowote kuwa anamiliki mali au akaunti yoyote ndani na nje ya nchi atangaze vitu hivyo kwani ukweli ni kwamba hana vitu hivyo kwani hata akienda kwao Kigoma anafikia kwa baba yake kama mtoto wa shule.
Edna posted 3/7/07 9:12 AM    
Written by Maxence M. Melo,,,,,,,, Sunday, 26 March 2006 ,,,,,,,, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe amesema atawashtaki na kuwadai fidia ya Sh. milioni 1,000 watu 'wanaompakazia' na kumshutumu kuwa amejilimbizia mali nyingi... Akizungumza kwenye kipindi kinachorushwa kupitia vituo vya luninga vya StarTv na Channel 10 mwishoni mwa wiki, Askofu Kakobe alisema, kwa muda wa takribani miaka 14 sasa, kumekuwepo watu wanaoeneza uzushi kuwa anamiliki mali nyingi, habari alizosema kuwa hazina ukweli wowote. Katika kudhihirisha anaishi katika hali ya umaskini na dhamira ya kumtumikia Mwenyezi Mungu, Askofu Kakobe alionekana katika luninga hizo akiionyesha nyumba anayoishi huko Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huku akiwa ameshika Biblia na kutembea kwa mwendo wa polepole, Askofu Kakobe alionekana akifungua geti la kuingilia nyumbani kwake na kuonyesha vyumba na mali zilizomo ndani yake. Ndani ya chumba chake, Askofu Kakobe alionyesha kabati la kuhifadhi nguo alilolinunua miaka mingi iliyopita, ambalo hata hivyo alisema halitoshi kwa mahitaji ya hivi sasa, hali inayomfanya yeye na mkewe kuhifadhi nguo nyingine juu ya kitanda cha mtoto wao. Alisema, nyumba hiyo ndiyo pekee anayoimiliki na kuwa hata katika kijiji cha Kakonko mkoani Kigoma alipozaliwa na mahali wanapoishi wazazi wake, hajajenga nyumba ya aina yoyote. Pia Askofu kakobe alisema gari analolitumia hivi sasa, ni mali ya kanisa na kwamba yeye anamiliki pick-up mbovu inayoendelea kuozea nje ya nyumba yake. "Kwa nini wananivunjia heshima yangu? Ninawatahadharisha watu wote wanaovumisha habari hizi kwamba sasa nitachukua
Mshirika FGBF posted 3/7/07 12:46 AM    
Hapo mahakamani ndipo tulipokuwa tukipangoja sana ili tutoe ushahidi jinsi Kakobe anavyotuibia mali na hata wake zetu. Mabinti wanavalishwa vitambaa na kuambiwa ni lazima waombewe na mtumishi wa Mungu maombi maalum. Nyumba anayodai kuimiliki Kakobe ni kifunga macho tu. Tunajua kila kitu. Kwanza mliona wapi kanisa ambalo lina nyumba kulala mchungaji akiombea mabinti bila mke wake? Yote hayo tutayasema mahakamani. Wote waliofukuzwa kazi baada ya kutoa pesa na mali zao kwa Kakobe mtawaona mahakamani. Wengine walichukua mikopo makazini wakazileta pesa zote miguuni pa Kakobe, nae akawaahidi baraka hewa ambazo hawakuzipata. Tumelalamika miaka mingi serikali iingilie kati bila mafanikio. Sasa Kakobe anafikiri ameweka mambo sawa na yuko tayari kwenda mahakamani. Ni sawa na Twiga aliyeficha kichwa mchangani na kudhani kwamba haonekani. Hata kipindi chake kwenye TV ni utapeli mtupu. Utamsikia akisema kwamba ameoneshwa kupitia roho mtakatifu kwamba kuna watu wenye MMBA ambao Mungu atawaponya. Sasa ukiwakusanya watu mia mbili katika jiji la Dar karibu wote hawatakosa kuwa na mba za kichwani. Magonjwa ya ngozi ni mengi Dar. Kuwatapeli kwamba Bwana amewaponya na hakuna thibitisho toka kwa Daktari, Huo ni utapeli unaofanyika mchana kwenye TV na serikali ikiona bila kumchukulia Kakobe hatua za kisheria. Isitoshe watu hao wataambiwa wapande mbegu ili wavune. WIZI UKO HAPO. Wanatoa na hawabarikiwi. Wakiishiwa na kuwa masikini wanaondoka kimya kimya. Kanisa linapaswa kuwafundisha watu jinsi ya kufanya kazi kwa bidii, na siyo kuwapokonya kidogo walicho nacho na kumkabithi Kakobe. Wengine wamesema hapa kwamba Kakobe ni mfanyibiashara maarufu na siyo mtumishi wa Mungu. Alianza na kampuni yake ya MULANGA EDITION ambayo ilikuwa ikinakili nyimbo za wasanii kutoka santuri na kuziweka kwenye kanda bila kibali cha wasanii husika. Wakati sheria za kimataifa za hatimiliki zilipoanza kufanya kazi, Kakobe aliachana na kazi hiyo japo alikuwa amechuma pesa nyingi sana kwa kazi yake hiyo haramu. Wakati wote huo Kakobe alikuwa akijiita MLOKOLE. Tena alikuwa akitumia pesa hizo haramu kuandaa mikutano ya Injili TEMEKE TAG kwa sasa TEMEKE EAGT. Wao na kulola walikuwa pete na kidole kwani Kakobe alionekana mwenye pesa wasijue alikuwa akiwaibia wasanii. Ukisoma magazeti ya UHURU ya mwaka 82-86 utaona jinsi Kakobe alivyokuwa akiihalalisha kampuni yake hiyo haramu kwa kuitangaza kwenye vyombo vya habari. Hata sasa anatumia mbinu hiyo hiyo. Kanisa lake lina mengi sana ya siri ambayo tutayafichua mahakamani. Tofauti na makanisa mengine ya walokole yanayoamini kwamba kila mtu aliyeamini Injili anapewa uwezo wa kufanyika Mwana wa Mungu, Kwa Kakobe mtumishi ni yeye na wengine ni wa kuhudumiwa. Yaaani daktari wa kiroho ni Kakobe na washirika wote ni wagonjwa wanaosubiri kumuona Kakobe wasaaidiwe mahitaji yao ya kiroho na kimwili. Hayo ni mafundisho potovu ambayo serikali inapaswa kuyatupia darubini kwani madhara yake ni pale watu watakapoibiwa bongo zao kiasi cha kuambiwa leo Mungu anataka wote twende mbinguni kwa njia ya kujiua na washirika wote kukubali bila kuuliza swali. Kakobe anaelekea hapo.
Edna posted 3/8/07 10:41 AM    
Pole sana wewe unayejiita Mshirika wa FGBF church, kwa kuchukuliwa mkeo na Mtumishi wa Mungu kakobe, je! mkeo alikuambia kuwa aliitwa kwenye chumba cha siri kuombewa na kakobe harafu , ikawa si mamombi akamgeuzia kibao? Na umesema na mabinti zenu pia hufanyiwa hivyo, je! na binti yako alikusimulia? Na baada ya kupatwa na mkasa huo ulichukua hatua gani, kwa mkeo na hata kwa binti yako? Au ndiyo unasubiri siku mkifikishana mahakamani na Kakobe ndiyo umshtaki? au hayo umesimuliwa tu wewe hayajawahi kukupata? na kama ndiyo una uhakika gani kuwa kakobe anawafanyia hivyo wanawake na mabinti? mmmh! hizi ni nyakati za mwisho tuweni makini sana. Wapinga kristo si mpaka akwambie Yesu si Mungu, wapo humu humu makanisani tunasali nao. Na wewe kama unamshtumu Kakobe, bado unafanya nini kanisani humo? unaenda kusali nini kama haumuamini huyo mtumishi?
Mshirika FGBF posted 3/8/07 1:23 PM    
Yatakapotokea mtasema nilisema. Kwa KAKOBE neno lake ndio mwisho. Yeye ni zaidi ya Mussa. Hata wana wa Israel walijaribu kumhoji Musa awaache na wenyewe waende kuzungumza na huyo Mungu.Yaliyotokea yanaeleweka. Wakati huo NEEMA ilikuwa bado. Je hata sasa baada ya kiambaza kuvunjika kuna watu wanaofanya kazi ya udalali kwa Yesu? Kwa nini basi nilitoka KATOLIKI? Nilitoka niwe huru kwenda kwa Mungu na kumuomba msamaha bila kupitia kwa PADIRI kila ijumaa. Kama hata huku kwa KAKOBE mambo ni yale yale ya KATOLIKI, si bora watu warudi KATOLIKI maana huko kidogo hata kama wanafanya madhambi yao hawayafanyi peupe kama kina KAKOBE. Yani nina maana PADIRI atavaa kanzu ambayo KAKOBE havai,Kanisani watawasha mishumaa ambayo kwa KAKOBE hawawashi, Tena KATOLIKI kuna sanamu ya Yesu na BIKIRA MARIA ambazo kwa Kakobe hakuna. Kwa hiyo kama watu wanataka kuhudumiwa kiibada basi warudi KATOLIKI kuliko kutapeliwa kwa KAKOBE.Kwanza YEYE anafikiri akivaa suti ambayo kila mtu huvaa itamfanya mtumishi wa Mungu. Maana yangu hapa ni kwamba WALOKOLE MATAPELI wanafanya hivyo kwa njia ya chini sana kila mtu mwenye akili timamu atawagundua.Kinachonishangaza ni kwa nini wengine hawaoni nionavyo. Wengi bado wanamuogopa KAKOBE kiasi cha kuogopa kuyataja mabaya waliyofanyiwa hadharani. Kakobe anawatisha kwamba atawalaani. Kazi yangu kubwa sasa ni kuwaondoa hofu hiyo ili tukifika mahakamani tuseme kila kitu. Wengi mtashangaa mtaka[poyasikia. Ni mengi yanatisha na watanzania hawatayaamini masikio yao. Tayari kuna mchungaji mmoja ambaye amehukumiwa kwenda jela kwa kosa la kuchangisha pesa ngambo kwa njia ya utapeli. Mbona serikali haiwaoni hawa wanaochangisha pesa hapa nchini na kuzitumia kwa malengo tofauti na injili? Mfano kipindi cha TV anacholipia KAKOBE STAR TV. Huu ni ufujaji wa pesa kwani kipindi hicho huchangiwa na washirika ili aonekane KAKOBE pekee akiwahudumia waliokichangia kipindi. Hiyo ni kinyume na maandiko. Neno la Mungu linasema kwamba mkutanikapo huyu ana zaburi na mwingine ana neno la maarifa na mwingine ana unabii. Kila mkristo aruhusiwe kuongea kwenye kipindi hicho. Hata kama ni dakika chache lakini kinaweza kuwajumuisha makundi mbalimbali kanisani ili kikose kuwa na KAKOBE kila wakati. Najua hapo nimemgusa PAHALA kwani hata makanisa ya mikoani anayoyaongoza, kila jumapili lazima waweke kanda ya KAKOBE. Mungu anaweza kuzungumza na watu walipo na siyo lazima atumie KAKOBE TUUUUUUU. Jambo jingine washirika wote tunapaswa kuwa wadau wa shughuli zote za kanisa. Mapato na matumizi ya pesa za kanisa yaidhinishwe na washirika na siyo KAKOBE na wazee wachache wanaosema ndiyo kwa kila jambo. Jingine ni suala la katiba ya KANISA isiwe ni siri ya KAKOBE. Tusomewe katiba ya kanisa letu, ikibidi tuibadili, na tuiwasilishe kwa msajili wa vyama ili tuwe na uchaguzi wa askofu. Haiwezekani KAKOBE awe mwanzilishi, Tena awe mmiliki, na sisi tuwe mali yake. HAPANA. Kanisa ni la jumuia husika. Kama ulianzisha haikuwa na maana kwamba ni mali yako binafsi. Bado Kakobe analiongoza kanisa kama kampuni binafsi. Hilo ndilo tunalosema hatutaki.
Edna posted 3/9/07 12:58 AM    
Aisee! hii kali unataka kuniambia makanisa ya Mikoani ya FGBF hayana wachungaji wanayoyaongoza wanaweka kanda tu??? Mmh! nitafanya utafiti nitatafuta kanisa lake mahali kisha nitaenda kuhakikisha kama ni ukweli kwa sababu tusipende kusimuliawa bali kuwa na hakika.Na kitu kingine mimi sintapenda kubisha sana kwa hayo uyasemayo ya kumuhusu Kakobe kuwa ni Tapeli, kwa sababu sijawai sali hilo kanisa na wala sijawahi ingia katika mlango ule. Na yamkini wewe unalalamika kwa sababu yamekukuta , nikimaanisha na wewe ni sehemu ya watu waliotapeliwa mali zao na Kakobe.Nasema siwezi pinga kabisa, kwa sababu hata mimi nishawahi tapeliwa na mtumishi fulani ambaye , mwanzo sikujua kuwa yeye ni tapeli amefanya dini kama biashara ya kujiingizia kipato. Nilimuamini sana na nilimpa pesa zaidi ya Milioni moja (1,000,000/=), zilikuwa zangu na zingine alidiriki kusema nikaanzime mahali, nikaingia deni la laki 800,000/= kwa watu tofauti tofauti nikamkabidhi.Mmoja alinipa laki 6 na mwingine laki 2. Na baadaye wala asilipe hilo deni na kukimbilia Mwanza, nimeshindwa hata kumshtaki kwa sababu uaminifu wangu kwake kama yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana ulinifanya nisiandikishiane zile pesa, kwa hiyo nimemuachia Mungu kwa sababu hata kama nikisema nikamshtaki sina kithibitisho.Ni kweli dunia imeharibika siwezi mtetea Mtumishi yeyote wa Mungu ninaposikia mabaya yake, kwa sababu sijui undani zaidi yake huo ndiyo ukweli.Kwa hiyo nimeingia kwenye deni ambalo sikutegemea, lakini Mungu hawezi mpa mtu jaribu lisilokuwa na mlango wa kutokea na linalomzidi uwezo mjaribiwa. Mtu aliyeniazima laki 6, amenisamehe deni, na si kwamba yeye ni tajiri hapana bali ni Mungu tu amefanya njia kwa sababu alijua ya kuwa hilo jaribu litanishinda uwezo, nitashindwa kulipa hilo deni, na bado na kwa mtu aliye niazima laki 200,000/= ni deni ambalo naweza kulilipa, huyo ndiyo Mungu.Pole sana Mshirika wa FGBF. Ila nataka kujua bado unaendelea kusali kwenye hilo kanisa kila j2 au???????
Mshirika FGBF posted 3/10/07 10:42 AM    
Kumbe tuko wengi. Pole EDNA. Kama kila aliyetapeliwa angejitokeza na kusema tu, ingetosha kuwafanya hawa matapeli wajue kwamba watu wamewashitukia. Wengi wanaogopa kufanya hivyo eti wasionekane kuwanyooshea kidole wapakwa mafuta ya roho mtakavitu. Wengi wanaibiwa kimya kimya. Kila kanisa lenye roho hiyo, lazima mchungaji atakuwa na mipango inayozidi kiwango cha mapato ya washirika wake. Washirika ambao hawawezi kumudu milo mitatu kwa siku wanatakiwa wachange ili mchungaji awe na mamilioni ya pesa azitumie apendavyo. Kipindi cha KAKOBE STAR TV kinagharimu mamilioni ya shilingi kila kinaporushwa hewani. Pesa hizo tunalipa sisi washirika. Watoto wetu wanafukuzwa shule kwa ukosefu wa karo. Pesa zote tunaleta kanisani. Mavazi hatuwezi kumudu. Mchungaji kila siku anabadili suti. Na zote hizo ni pesa zetu. Mchungaji Kakobe hawezi kupanda basi au Treni kwenda mikoani. Lazima apande ndege. Hizo ni pesa zetu. Utamsikia Kakobe amemwalika KULOLA na amempa zawadi za mamilioni ya pesa. Zote hizo ni pesa zetu. Wakati kuna washirika wanaolala njaa siyo kwamba wana saumu, HAPANA hawawezi kumudu chakula cha kila siku. Pesa za kanisa zilipaswa kuyaangalia kwanza mahitaji ya washirika kusiwepona mshirika mwenye mahitaji. Hiyo ndiyo biblia inavyozuyngumza kuhusu matoleo. Matoleo hayakupaswa kumtajirisha mchungaji huku washirika wakibaki masikini wa kutupwa.Kinachotokea ni wachungaji kujiingiza kwenye miradi isiyolingana na kipata cha washirika wake. Matokeo ni washirika kulazimika kukopa ili kumudu mahitaji ya mchungaji yasiyokoma. Sasa basi. Wakuondoka ni Kakobe siyo sisi tunaomwambia kweli. Kanisa ni mali ya Yesu na siyo la KAKOBE. Bado niko kanisani, wakuondoka ni KAKOBE siyo mimi.
Kaduguda! posted 3/20/07 7:58 PM    
Hapa tunadanganyana, hakuna cha mshirika wa FGBF wala nini. Ninachokishuhudia hapa ni uongo mtupu. Huyu sio mshirika bali tapeli tu aliyetumwa na Shetani kuwarubuni watu wa Mungu kwa kujifanya mshirika! ANA ROHO NYEHU muogopeni!
Abel A. Kinyondo posted 3/20/07 8:13 PM     Click here to send email to Abel A. Kinyondo  
Huyu Kakobe amesemwa vya kutosha na cha kushangaza hakuna ushaidi kamili wa kumwonyesha kwamba ni waupotevuni. Napajua hadi kwao Kakonko, Kibondo, Kigoma. Hakuna cha kutazamika kabisa. Ok naweza nisijue nini kinaendelea kanisani kwake lakini jamani kuliko kupoteza muda kuponda wachungaji kwa nini basi sisi akina MUNISHI tusionyeshe namna mchungaji mwema anatakiwa awe. Mtajikuta mnajinajisi na kujipa laana bila sababu ya msingi. WALOKOLE tuangalie hata haya tunayoongea hadharani. Kwa mwendo huu sijui hata wapagani wanaosoma hii website kama wataokoka.
Edna posted 3/23/07 11:53 AM    
Kaka Abel.A Kinyondo nimesoma jinsi ulivyo comment, na si kwamba namuunga mkono mshiriki wa Kakobe anavyoongelea kuhusu wanavyotapeliwa hapana. Yeye binafsi na Mungu pekee ndiyo wanaujua ukweli. Ila ukisema kuwasema Watumishi matapeli ni kuwafanya watu wasiokoke, ni kweli ila si aslimia 100, kwa sababu penye ukweli lazima tuongee kama mimi nilivyoelezea hapo juu, kweli yalinikuta na nilitapeliwa. Na hata biblia inasema si wote wasemao bwana bwana wataurithi ufalme wa Mbinguni.Ni bora watu wajue kuwa kuna watumishi matapeli, na kuokoka kwa mtu ni neema ya Mungu tu, hataki mtu apotee bali kila mmoja aifikie toba. Kuna watu wangapi wanapinga wokovu ila baadaye wanakuwa wa kwanza kumtangaza kristo, hiyo ni pale neema inapowashukuia. Ila mimi nilikuwa naomba watu wanaoanzisha mada hizi wawe wanafikiria kwanza, si kusema mabaya tu ya watumishi bali hata kuanzisha mada za kumtangaza kristo. Mungu anisamehe kama kuna mahali nimekosea katika kuchangia mada hii.Sina nia mbaya na watumishi ila kweli wapo matapeli tena wengi, nikimaanisha Ma agent tunao wengi tu hata biblia inasema.
MAN posted 3/4/08 11:57 PM    
me naona huu ni unafiki mtu kama kuna mtu una ona anafanya kitu kinyume kusanywa masahidi mfuate huo ndio ukristo
Abdulwahid posted 3/22/08 9:50 PM    
Natamani nikutane na huyu chizi anayejiita mshirika wa FGBF ili nipate kumsaidia jinsi ya kufika FGBF ili apate toba na uponyaji wa akili yake aondokane na uchizi alionao. Jamani au nyinyi wengine hamuoni kama huyu ni miongoni mwa waliopata matatizo baada ya kutukana watumishi wa Mungu hebu nitafutieni mtu huyu jamani, anateseka.
Return To Message Board

http://munishi.com  | Post New Topic